SIKU MOJA KABLA YA UCHAGUZI JUCO,ABUI MKUMBO AZUA MASWALI MIONGONI MWA WANAFUNZI

 

Na Jey Future TZ – Future MEDIA Update

Kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi zimehitimishwa rasmi leo katika hali ya shamrashamra na mvuto mkubwa. Wagombea wote waliwasilisha sera zao mbele ya wanafunzi waliokusanyika kwa hamasa kubwa, isipokuwa mgombea Abui Mkumbo ambaye hajajitokeza kunadi sera zake hadi sasa, bila maelezo rasmi kutoka kwa uongozi wala timu yake ya kampeni.



 Daniel Augustino ameibuka kama mgombea mwenye uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanafunzi, akifuatiwa kwa karibu na Vitor Kajoro. Bahati Makoi naye ameleta ushindani kwa kutoa sera tofauti na zenye mvuto mkubwa kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi.

 Upigaji kura unatarajiwa kufanyika kesho, huku maandalizi yakiwa tayari kukamilika. Tume ya uchaguzi imeahidi kutangaza matokeo mapema zaidi ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka uliopita wa 2023/2024.

 Fuatilia Future MEDIA kwa matokeo ya moja kwa moja na taarifa zote muhimu kuhusu uchaguzi huu wa kihistoria.












Comments

Popular Posts