ALIO UKOSA BABA ATAPEWA MTOTO
ZANZIBAR — KATIKA hekaheka za maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, klabu ya Simba imedhihirisha dhamira yake ya dhati kuhakikisha historia haijirudii. Ni dhamira iliyojaa heshima, kumbukumbu na kiu ya mafanikio ambayo yamecheleweshwa kwa zaidi ya miongo mitatu.
Mnamo mwaka 1993, Simba ilifika hatua ya fainali ya mashindano ya Afrika, na mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Bara. Lakini, kama ilivyoandikwa katika historia, Simba walishindwa kunyakua ubingwa huo mbele ya macho ya kiongozi huyo, jambo lililowaumiza mashabiki wengi, hasa kutokana na heshima waliyotaka kumpa kiongozi wao kupitia ushindi.
Miaka 32 baadaye, historia inaandika ukurasa mwingine. Simba imetinga tena fainali, safari hii wakikabiliana na RS Berkane ya Morocco. Wanalazimika kushinda kwa mabao 3-0 ili kulibakisha kombe hilo nyumbani. Mchezo huo wa marudiano utafanyika Jumapili, Mei 25, 2025, Uwanja mpya wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Katika kuonyesha uzito wa mchezo huo, uongozi wa Simba ulifanya dua maalum walipotembelea kaburi la Hayati Ali Hassan Mwinyi lililopo Manga Pwani, Visiwani Zanzibar. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema. imeandaliwa na Jeremia emanuel
Comments