AMUUA BABA YAKE MZAZI KWA KUMKATA PANGA KICHWANI

 


 Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limemkamata Ayubu Rashid Ayubu (23) mkulima mkazi wa Gang'anda kwa tuhuma ya kumuua baba yake mzazi aitwaye Rashid Ayoub Juma (71) mkulima mkazi wa Gang'anda kwa kumshambulia na Panga eneo la kichwani upande wa kisogoni.

Taarifa ya leo Mei 30, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro SACP. Alex Mkama imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Mei 29, 2025 asubuhi katika kitongoji cha Gang'anda kijiji cha Mifuru kata ya Tegetero wilaya ya Morogoro huku chanzo cha tukio hilo likitajwa kuwa ni changamoto ya afya ya akili.

    Taarifa hiyo imebainisha kuwa marehemu akiwa amepumzika nyumbani kwake, kijana wake, kwa ghafla alianza kumshambulia kisogoni mithiri ya kukata mti na kusababisha kupoteza maisha huku jeshi la Polisi likitoa wito kwa Jamii kushughulikia kikamilifu changamoto mbalimbali za kijamii ili kuepuka matukio mabaya kama haya.


Comments