APOTEZA FAHAMU WAKATI AKIIBA NYAYA ZA UMEME

 


Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Rajabu Jumanne (21) mkazi wa kijiji cha Njirii wilaya ya Manyoni mkoani Singida, amenusurika kifo baada ya kupigwa shoti ya umeme hadi kupoteza fahamu, wakati akiiba nyaya za umeme kwenye Transfoma ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) iliyopo katika kijiji hicho. 

Inadaiwa kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Mei 28, 2025 kijijini humo ambapo kijana huyo alikutwa akiwa amepoteza fahamu baada ya kufanya jaribio hilo la wizi na alipohojiwa alikiri kwamba amekua akifanya matukio ya aina hii mara kwa mara kwenye maeneo tofauti.

"Nilimuhoji akasema ni kweli nilikuja hapa kwaajili ya kuiba nyaya za 'Copa' na nikisha iba nazisafirisha kupeleka mwanza, matukio haya sifanyi hapa tu mimi ni mzoefu huwa nafanya matukio haya sehemu tofauti" Mtendaji wa kijiji cha Njirii Adam Mkwavi akizungumzia tukio hilo.

Comments