LAMECK HAULE ATENGULIWA KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS KATIKA CHUO KIKUU JORDAN (JUCO)
Na: Jeremia emanuel – Morogoro
Morogoro, Mei 27, 2025 — Mgombea wa nafasi ya urais katika serikali ya wanafunzi wa Jordan University College (JUCo), Ndg. Lameki Haule, ametenguliwa rasmi kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kutokana na sababu zilizotajwa kuwa ni "za kiutawala".
Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi, tarehe 24 Mei 2025, ambapo wagombea wote wa nafasi ya Urais na wenza wao waliitwa na uongozi wa chuo kwa ajili ya kupatiwa mrejesho kuhusu hatua ya mchakato wa uchaguzi.
Katika taarifa rasmi aliyoitoa kwa umma kupitia ujumbe wa timu yake ya kampeni, Haule alieleza kwa masikitiko kuwa jina lake pamoja na mwenza wake, Bi. Beatha, yalienguliwa na chuo kwa maelezo ya kiutawala.
"Siku ya Jumamosi, tarehe 24.05.2025, wagombea na wenza wao katika nafasi ya Urais tulitwa na kupewa mrejesho kutoka Utawala wa Juco. Kwa bahati isiyo njema, nasikitika kuwatangazia kuwa majina yetu; Ndg. Lameck na Beatha yalitenguliwa katika nafasi hiyo kwa sababu za kiutawala," alisema Lameck katika taarifa hiyo.
Licha ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro, Haule alitoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kipindi cha maandalizi ya uchaguzi na kueleza msimamo mpya wa timu yake wa kutokata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
"Baada ya kukaa kwa pamoja, kamati yetu imeazimia yafuatayo:
kutokata rufaa, kuwapa wafuasi wetu uhuru wa kujiunga na upande wowote, na kamati imependekeza kumuunga mkono Ndugu Bahati na Tausi katika nafasi ya Urais," alisema Mgombea.
Haule alihitimisha taarifa yake kwa kuwatakia heri wagombea waliobaki kwenye kinyang’anyiro huku akiashiria mshikamano wa kweli na wito wa kuendeleza amani, umoja na ushirikiano ndani ya jamii ya wanafunzi wa JUCo:
"Together We Can, Together We Win."
Mwisho
Kwa taarifa zaidi kuhusu uchaguzi wa serikali ya wanafunzi JUCo, endelea kufuatilia FutureMediaupdate
Comments