MALIPO YA AZIZ KI WYDAD YAFICHUKA – MAMILIONI KILA SIKU!

 

   Mchezaji mahiri wa kimataifa kutoka Burkinafaso , Stephane Aziz Ki, sasa ni mali ya klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco, baada ya kukamilisha usajili wake rasmi akitokea Yanga SC ya Tanzania. Usajili huu unatajwa kuwa mmoja wa mikataba ya kihistoria kwa mchezaji aliyecheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Aziz Ki amesaini mkataba mnono ambao utakuwa ukimpatia Tsh Bilioni 1.2 kwa mwaka, kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwa mchezaji aliyeondoka ligi ya Tanzania kwenda kwingine barani Afrika.

Malipo ya Aziz Ki kwa mujibu wa mkataba wake mpya ni kama ifuatavyo:

💰 Bilioni 1.2 kwa mwaka

💵 Milioni 107 kwa mwezi

💸 Milioni 3.5 kwa siku

⏱ Shilingi 2,442 kwa kila dakika

Usajili huu ni ishara ya thamani kubwa aliyoijenga Aziz Ki ndani ya muda mfupi akiwa na Yanga, ambapo aliibuka kuwa mchezaji tegemeo, nahodha na kiungo anayeongoza kwa ubunifu na mabao muhimu katika mechi kubwa.

Mashabiki wa Yanga wamepokea taarifa hizi kwa hisia tofauti – wengi wakimpongeza kwa hatua kubwa ya mafanikio, huku wengine wakihisi pengo kubwa litakalosababishwa na kuondoka kwake.

Wydad, klabu tajiri na yenye historia kubwa barani Afrika, imeonyesha dhamira ya dhati ya kurejesha makali yake kwa kumleta nyota huyu ambaye atakuwa na jukumu la kuimarisha safu ya kati na kusaidia timu katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa kama CAF Champions League.

#AzizKi #Wydad #YangaSC #TransferNews #FootballAfrica #Usajili

Je, una maoni gani kuhusu uhamisho huu wa kihistoria? Tuambie kwenye comments.





Comments