MASAA MACHACHE YAMESALIA KABLA YA KUTANGAZWA KWA KAMPENI ZA UCHAGUZI 2025 (JUCO)


 Morogoro, Tanzania – Mei 30, 2025

    Masaa machache kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Jordan (JUCo), matarajio na hamasa vimepamba moto miongoni mwa wanafunzi. Uchaguzi huu wa mwaka 2025 unatarajiwa kuwa wa kipekee, ukionyesha ongezeko la ushiriki wa wanafunzi na ushindani mkali kati ya wagombea.

  Kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi kesho, Mei 31, 2025, zikihusisha midahalo ya wazi, mijadala ya sera, na matumizi ya majukwaa ya kidijitali kwa ajili ya kuwafikia wapiga kura. Vyombo vya habari ikiwemo #FutureMedia, vitahakikisha taarifa sahihi na kwa wakati zinawafikia wanafunzi wote.

Uchaguzi wa mwaka 2025 katika chuo kikuu Jordan University College unatarajiwa kuwa wa kihistoria, ukiashiria ongezeko la ushiriki wa wanafunzi na ushindani wa kweli. Wanafunzi wote wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika kampeni na hatimaye kupiga kura kwa ajili ya mustakabali bora wa chuo.







Comments