MBOWE AVUNJA UKIMYA ATOA LA MOYONI..
Mwenyekiti wa zamani wa #CHADEMA, #FreemanMbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu Uchaguzi Mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025 ulipomalizika, akidai wanaotakiwa kuzungumza kwa sasa ni Viongozi waliokabidhiwa Mamlaka na chama
Mei 19, 2025, alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, alijibu “Niseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka.... wasije wakadai tunawashwawashwa.”
Ikumbukwe Mei 18, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob “Boni Yai”, alitangaza hana mpango wa kuhama chama, akadaia anaamini baadhi ya Makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe hawajatumwa na Mwanasiasa huyo.
Soma kupitia https://futuremedia123.blogspot.com
Comments