MOTO WA UCHAGUZI WAANZA KUWAKA JUCO JE, NANI KUTWAA TENA KITI HIKI CHA MOTO MWAKA HUU?
Imeandaliwa na jey future Tz;
Moja ya chaguzi zilizobeba uzito mkubwa katika historia ya serikali ya wanafunzi wa Jordan University College (JUCo) ni uchaguzi wa mwaka jana wa 2024/2025. Uchaguzi huo uliingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa na idadi kubwa ya wagombea na kampeni zilizokuwa na mvuto mkubwa ndani na nje ya CHUO
Mchuano huo ulijumuisha wagombea maarufu kama Alimia Libela, Grinesi Sichone, Chacha, na Elisha Ntasubila. Hata hivyo, awali, vita vya kisiasa vilionekana kuwa kati ya Grinesi Sichone na Alimia Libela.
Hali hiyo ilibadilika ghafla baada ya kuibuka kwa kijana mwenye ushawishi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii, Jey Future Tz, ambaye kwa wakati huo alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.Kupitia nguvu ya mabadiliko ya kimtandao, Jey Future Tz alifanikiwa kuhamasisha wafuasi wengi na kusababisha ushindani kugeuka kati ya Chacha na Grinesi, hali iliyotikisa kabisa mwelekeo wa kampeni. Pamoja na mikikimikiki hiyo yote, mwishowe Alimia Libela aliibuka mshindi na kutangazwa rasmi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi JUCo.
Sasa, baada ya miezi kadhaa kupita, macho na masikio ya wanafunzi na wadau wa chuo yameelekezwa kwa uchaguzi wa 2025. Swali kubwa linalotawala vichwani mwa wengi ni "Je, nani atatwaa kiti hicho moto safari hii?" Je, kutakuwa na sura mpya au mmoja wa waliowahi kugombea atarejea kwa kishindo?
Dalili zinaonesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa wa kusisimua zaidi, huku majina mapya yakianza kusikika kwa sauti ya chini na mitandao ya kijamii ikiwa na nafasi kubwa zaidi katika kuelekeza upepo wa kampeni.
Kwa sasa, jamii ya wanafunzi inaendelea kusubiri kwa hamu majina yatakayojitokeza, huku midahalo, kampeni na mivutano ya hoja ikitarajiwa kuanza wakati wowote.
Je, historia itajirudia au itavunjwa? Muda utaongea.
Comments