MTOTO WA MIAKA KUMI AKAMATWA KWA WIZI WA GARI MOROGORO
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linaendelea na uchunguzi wa tukio la kushangaza la mtoto mwenye umri wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la tano aliyekamatwa akiendesha gari.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, tukio hilo limetokea asubuhi ya Mei 26, 2025 katika eneo la Kigurunyembe, Wilaya ya Morogoro ambapo Mtoto huyo alikamatwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 807 BVV, aina ya Toyota Spacio linalomilikiwa na Zuhura Khatibu (47), mwalimu na mkazi wa Kilakala mkoani Morogoro.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo, akiwa na wenzake ambao bado wanatafutwa na vyombo vya usalama walitumia funguo bandia kufungua na kuendesha gari hilo.
Kamanda Mkama ameeleza kuwa taarifa kamili kuhusu tukio hilo itatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Imeandikwa na Jeremia emanuel.
Comments