MWANDISHI MAHIRI NGUGI WA THIONG'O AFARIKI DUNIA
"Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha baba yetu, Ng农g末 wa Thiong'o, asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 28 Mei 2025. Aliishi maisha kamili, alipigana vita vizuri. Kama ilivyokuwa matakwa yake ya mwisho, tusherehekee maisha na kazi zake,"
Ng农g末 alizaliwa tarehe 5 Januari 1938 katika kijiji cha Kamiriithu, karibu na Limuru, Kenya. Alianza elimu yake katika Shule ya Sekondari ya Alliance na baadaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, ambako alihitimu mwaka 1963 na shahada ya Kiingereza.
Aliandika na kuigiza tamthilia yake ya kwanza, The Black Hermit, kazi zake nyingine ni pamoja na riwaya maarufu kama Weep Not, Child (1964), The River Between (1965), na A Grain of Wheat (1967) na nyingine nyingi
Ng农g末 wa Thiong'o ameacha urithi mkubwa katika fasihi ya Kiafrika, Riwaya zake kama Petals of Blood, Matigari, na Wizard of the Crow zimesomewa ulimwenguni kote na kutumiwa katika mitaala ya Elimu kufundishia.
Comments