RAIS SAMIA ASIKIA KILIO CHA MWALIMU YUSUPH AHAIDI KUMSAIDIA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kumsaidia mwalimu Yusuph wa Kigoma baada ya kuitazama makala fupi aliyofanya na @khaan_mbarouk hivi karibuni.

Rais @samia_suluhu_hassan ameweka ujumbe kwenye video aliyoiweka Khaan kwenye instagram yake unaosema “Nimepokea ujumbe. Nimevutiwa na ujasiri wake, bidii, kujitoa na kutokata tamaa. Hongera pia kwa mwenza wake kwa kudumu pamoja katika hali zote. Maisha huja na baraka na mitihani yake. Nitamsaidia. Wasaidizi wangu watawasiliana naye”

Comments