RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI JUCO ALIMIA LIBELA ATOA KILA LAHERI KWA WAGOMBEA WOTE WANAO WANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UCHAGUZI JUCO

 



Rais wa serikali ya Wanafunzi Jordan university college(JUCSO 2024/2025) Alimia Libela.Ametoa salamu za heri na mafanikio kwa wagombea wote waliotia Nia katika Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika hivi karibuni chuoni hapo.

Akizungumza na #Futuremediaupdate , Rais Libela aliwahimiza wanafunzi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya wengi na kuwa na dira ya maendeleo kwa jamii ya wanafunzi.

Pia alielezea mafanikiio mbalimbali katika serikali yake Ambapo amesema kwamba "Tumefanikisha mengi katika kipindi hiki, lakini mojawapo ya mafanikio makubwa kabisa ni ujenzi wa barabara inayotumiwa na wanafunzi kupitia geti namba nne, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa kero na changamoto kubwa," alisema Rais Libela.

Aidha, alitaja mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa huduma kwa wanafunzi, ushirikiano mzuri na uongozi wa chuo, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika shughuli za kijamii na kielimu.

Rais Libela alihitimisha kwa kutoa rai kwa wanafunzi kuwa na mshikamano na kudumisha amani wakati wa kipindi cha uchaguzi, akisisitiza kuwa uchaguzi ni fursa ya kukuza demokrasia na kuendeleza maendeleo ya chuo kwa ujumla.

Imeandikwa na, Jeremia emanuel wa Future Mediaupdate.



Comments