RAIS SAMIA AKELWA NA WANAOVUJISHA SIRI ZA SERIKALI
#dodoma: Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na baadhi ya watumishi wa umma ambao huvujisha siri na nyaraka za serikali akisema huko ni kukosa uzalendo kwa nchi. Rais Samia alitoa kauli hiyo mwishoni mwa juma hili wakati akiwaapisha baadhi ya watendaji aliowateua, na kuongeza kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakikiuka miiko ya utumishi na kukosa uzalendo hadi kufikia hatua ya kutoa siri za maeneo wanayofanyia kazi. Kauli yake imezusha mjadala kuhusu suala zima la uzalendo.
Comments