SAINI YA KIBALI CHA MAZIKO YALETA UTATA
#HABARI Vurugu zimeibuka na kudumu zaidi ya saa kumi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mwea Mission iliyopo huko Karira, Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya ambapo wanawake wawili na watoto wao kumi walikuwa wanazozana na kugombania nani atie sahihi kibali cha maziko ya mume wao.
Marehemu Francis Muthike, kutoka kijiji cha Mugaa wadi ya Mutithi, alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, akiwaacha wake zake wawili, Jane Wamwirua na Jane Wangeci, pamoja na watoto wao kumi.
Mzozo huo ulihusu nani alikuwa na haki ya kisheria ya kusaini kibali cha mazishi, ambacho walidai ni urithi muhimu wa mali. #FutureMEDIAUpdate
Comments