UGANDA YASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE ZA KIJESHI NA UJERUMANI
Hapo awali, jeshi la nchi hiyo lilishutumu baadhi ya balozi za Ulaya kwa kuunga mkono "makundi hasi na wasaliti", likimutenga balozi wa Ujerumani Matthias Schauer.
Ilifuatia ripoti kwamba wanadiplomasia walikosoa tabia ya mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mkuu wa jeshi.
Kainerugaba, ambaye anatajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kumrithi babake mwenye umri wa miaka 80 kama rais, anajulikana kwa machapisho yake yenye utata kwenye mitandao ya kijamii.
Imeandaliwa na Jeremia emanuel
Comments