AIT-NOURI KWA KARIBU KUJIUNGA NA MAN CITY KWA £31 MILIONI KUTOKA WOLVES
Manchester City karibu kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Rayan Ait-Nouri kutoka Wolves kwa £31m
Manchester City wako karibu kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Rayan Ait-Nouri kutoka klabu ya Wolves kwa dau la pauni milioni 31.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mwishoni mwa wiki hii kama hatua ya mwisho ya dili hilo, ambalo pia linajumuisha nyongeza ya pauni milioni 5 kama bonasi.
City watalazimika kukamilisha usajili huo kabla ya tarehe 10 Juni ili Ait-Nouri aweze kuwa sehemu ya kikosi katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la Klabu.
Ait-Nouri, ambaye ni raia wa Algeria, alikuwa chaguo la juu kabisa kwenye orodha ya kocha Pep Guardiola kutatua tatizo la muda mrefu kwenye nafasi ya beki wa kushoto.
Manchester City imekuwa ikicheza bila beki wa kushoto wa asili tangu kuondoka kwa Benjamin Mendy, ambaye mara ya mwisho alichezea klabu hiyo mwezi Agosti 2021.
Comments