Biashara ya Siri ya Wachawi: Ndani ya Masoko Yenye Hirizi, Mafuvu na Tiba za Ajabu”

 


Soko hili linaitwa Marche des FĂȘticheurs au Akodesewa Fetish Market, linapatikana katikati ya mji mkuu wa Togo, LomĂȘ. NI soko maalumu kwaajili ya uuzaji wa vifaa mbalimbali vya kiganga, kichawi kama vile hirizi na matunguli yanayotumika katika kinga za kichawi na uponyaji.

Katika soko hilo lenye meza nyingi zilizopambwa kwa ngozi za nyoka kumesheheni vifaa mbalimbali vya kiganga kama vile pembe, mifupa na mafuvu. Mbali na kuwa ni sehemu ya kuuzia vifaa hivyo, lakini pia kama unataka kutibiwa, kuagua ama kupiga ramli basi utahudumiwa ndani humo.

Soko kama hili pia linapatikana Lima Peru, ni soko lililofichwa sana, linaitwa Mercado de Brujas. Huko pia vinauzwa vifaa vya tiba za kienyeji kama vile mafuta ya nyoka NK, soko hili linaendeleza mila za kale za jadi za watu wa Amerika kusini.

Maeneo mengine yenye masoko kama haya ni La Paz Bolivia, soko linaitwa Nuestra Señora de La Paz, Mexico pia lipo soko kama hili, linaitwa Mecardo de Sonora.

Comments