DANIEL AUGUSTINO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA URAIS SERIKALI YA WANAFUNZI JUCO


 Jordan University College (JUCo), Morogoro – Katika uchaguzi uliojaa hamasa, amani na ushiriki mkubwa wa wanafunzi, Daniel Augustino ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi baada ya kupata ushindi wa kishindo dhidi ya wagombea wenzake watatu.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa leo na Tume ya Uchaguzi ya Chuo, Daniel Augustino alipata kura 694, akiwapiku kwa mbali wapinzani wake:


• Bahati Makoi – kura 440


• Abui Mkumbo – kura 175


• Victa Kajoro – kura 124


Ushindi huu unaashiria imani kubwa waliyonayo wanafunzi kwa Daniel, ambaye aliwahi kuhudumu kama Spika wa Bunge la Wanafunzi 2023/2024, akijulikana kwa uadilifu, uwakilishi imara na matendo yenye matokeo chanya kwa jamii ya wanafunzi.


Baada ya kutangazwa mshindi, Daniel alishukuru wanafunzi wote kwa kumuamini na kuahidi kuendeleza maono ya utawala unaosikiliza, kushirikisha na kutenda. Aliahidi pia kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii ya wanafunzi kwa karibu.

Tume ya uchaguzi imepongeza mwenendo wa uchaguzi huo, ikisema kuwa ulikuwa wa haki, huru na uliozingatia misingi ya demokrasia ya wanafunzi.


πŸ“‘ #FutureMediaUpdate | Tunakupatia Kilicho Bora


Comments

Anonymous said…
Daniel mitano tenaπŸ€£πŸ€£πŸ™πŸ™
Anonymous said…
Blessed Jey future media