DIG KENYA ANG'ATUKA KUFUATISMA KIFO CHA ALBET OJWANG


NAIBU Inspekta Jenerali (DIG) wa Huduma ya Polisi Nchini Kenya, Eliud Kipkoech Lagat, ametangaza rasmi kujiondoa katika nafasi yake wakati uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kifo chenye utata cha mwanablogu ‘blogger’ Albert Ojwang ambacho kimezua hasira kubwa kitaifa, huku kukiwa na wito unaozidi kuongezeka wa kuwajibika kwa maafisa wa juu wa polisi.

Mwanablogu huyo alikamatwa baada ya kuchapisha madai ya ufisadi yaliyomhusisha Lagat, hasa kuhusu upangaji wa kimkakati wa maafisa ndani ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na vitengo vya trafiki—nafasi zinazodaiwa kuwa na uhusiano na udhibiti wa mapato na taarifa za kijasusi.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Lagat amesema uamuzi wake umetokana na uzito wa ofisi yake na maslahi ya umma yanayohusiana na kesi hiyo. "Leo nimeamua kujiondoa kutoka ofisi ya Naibu Inspekta Generali - Huduma ya Polisi ya Kenya, hadi kukamilika kwa uchunguzi," — amesema Lagat

"Majukumu ya ofisi hiyo yatatekelezwa kuanzia sasa na naibu wangu hadi uchunguzi utakapokamilika. Ninaahidi kutoa msaada wowote ambao unaweza kuhitajika kutoka kwangu wakati wa uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha.


Comments