EU YAZUIA NDEGE ZA TANZANIA KUTUA AMA KUTUMIA ANGA LA ULAYA


Umoja wa Ulaya umefunga anga lake kwa mashirika ya ndege yaliyosajiliwa Tanzania na Suriname. Ikimaanisha kuwa ndege yoyote iliyosajiliwa Tanzania haitaruhusiwa kutua, kuruka ama kupita juu la anga la Ulaya. 

Umoja huo umesema kuna dosari katika usimamizi wa usalama wa safari za anga kwenye nchi hizo mbili.

Kamishna wa Uchukuzi wa EU amesema Tanzania inapaswa kuchukua hatua za haraka kurekebisha dosari hizo.

Comments