GTI: Kampeni ya Kitaifa ya Kijani Inayoibadili Tanzania Kwa Vitendo"

 













Kampeni mpya ya Mazingira kuzinduliwa Rasmi nchini Tanzania kwa jina la Green Tanzania Initiative (GTI) – kampeni inayowaleta pamoja vijana kutoka kila kona ya nchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Kampeni hii, iliyoanzishwa na Wilson Biseko Japhet, inalenga kuzinduliwa rasmi mwezi Julai2025, ikiwa na malengo mahsusi ya kuchochea uhamasishaji wa mazingira kupitia elimu, vitendo vya upandaji miti, usafi wa jamii, na kampeni dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

🌍 Malengo ya GTI ni pamoja na:

• Kupanda miti milioni 1 kufikia mwaka 2030

• Kuanzisha klabu za mazingira katika shule na vikundi vya vijana

• Kuendesha kampeni za elimu na usafi katika mikoa yote

• Kujenga mfumo madhubuti wa taarifa na ufuatiliaji wa shughuli za mazingira

Kwa mujibu wa GTI, harakati hii inalenga kuwapa vijana jukwaa la uongozi na ushawishi katika sekta ya mazingira huku wakitambuliwa rasmi kama Mabalozi wa Mazingira. Wanaochaguliwa watakuwa na jukumu la kutoa elimu ya mazingira, kuongoza shughuli mbalimbali, na kuwahamasisha wengine katika jamii zao.

🟢 Sifa za Kujiunga kama Balozi wa GTI:

• Umri kuanzia miaka 16

• Mapenzi ya dhati kwa mazingira

• Uwezo wa kushirikiana na jamii

• Simu yenye WhatsApp kwa mawasiliano

• Kujaza fomu ya usajili (ya mtandaoni au kwa maandishi)

🏅 Mabalozi watanufaika na:

• Vyeti vya utambuzi rasmi

• Uzoefu wa kazi ya kijamii

• Fursa za kushiriki mafunzo, semina na miradi ya kitaifa na kimataifa

• Mtandao wa marafiki na viongozi wa mazingira kutoka Tanzania nzima

📲 Jinsi ya Kujiunga:

Tuma ujumbe WhatsApp kwenda namba: +255 765 621 941👉 Jumuisha jina lako, mkoa, wilaya na sababu ya kutaka kuwa balozi

💬 Kauli Mbiu Yetu:

"Tanzania Kijani Inawezekana!"

Kwa mahojiano au ushirikiano zaidi, tafadhali wasiliana na:

📧 greentanzaniainitiative@gmail.com

📱 +255 765 621 941





Comments