JOTO LA KAMPENI LAZIDI KUPANDA JUCO
Jordan University College (JUCO) iko katika hali ya joto kali la kisiasa kufuatia kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Tangu kutangazwa rasmi kwa tarehe ya uchaguzi siku ya Ijumaa iliyopita, hali ya ushindani imepamba moto huku wagombea wakuu wakivuta hisia za wanafunzi kila upande.
Wagombea wa nafasi ya urais ni Daniel Augustino, Victa Kajoro, Abui Mkumbo, na Bahati Makoi. Hadi sasa, ushindani mkubwa unaonekana kuwakutanisha wagombea wawili: Daniel Augustino na Victa Kajoro, ambao wameweza kujipatia uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wanafunzi kupitia kampeni zenye mvuto na ushawishi.
Ingawa upande wa Abui Mkumbo umeonekana kutokuwa na nguvu kubwa ya kisiasa, hoja zinazotolewa na mgombea huyo zimekuwa na mashiko na kutambuliwa na baadhi ya wanafunzi kama za msingi kwa maendeleo ya JUCO. Hali hiyo inaashiria uwezekano wa mvuto wa dakika za mwisho kama mikakati itaongezwa.
Kwa upande mwingine, Bahati Makoi hajajitokeza sana kwenye majukwaa ya kampeni ikilinganishwa na wenzake, Ja kuwa kiasi kikubwa ameonesha nguvu sana katika mitandao ya kijamii,jambo linalo tia wasiwasi kwa wagombea wengine katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kampeni zinatarajiwa kufikia tamati kesho siku ya Alhamisi, kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika siku ya Ijumaa, ambapo wanafunzi wa JUCO watatumia haki yao ya kidemokrasia kumchagua kiongozi wao wa juu.
Swali kubwa linalobaki kwa sasa ni: Nani ataibuka mshindi wa kiti cha urais mwaka huu wa 2025/2026? Wanafunzi na wadau wa maendeleo ya taasisi hiyo wanasubiri kwa hamu na shauku matokeo ya uchaguzi huo.
FUTURE MEDIA, Tutakuletea taarifa zaidi kadri hali itakavyoendelea.
Comments