JUCo Yasimama Kidete, Wanafunzi Wajitokeza kwa Kupiga Kura
Imeandikwa na jey future tz ;
Zoezi la upigaji kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Jordan University College (JUCo) limeanza rasmi leo, likishuhudiwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojitokeza kushiriki.Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amepongeza mwitikio huo na kutoa wito kwa wanafunzi wengine kuendelea kujitokeza kwa wingi. Aidha, alibainisha kuwa lengo ni kufanikisha zoezi hilo mapema iwezekanavyo huku akieleza kuwa maandalizi yamekuwa mazuri na mazingira ya upigaji kura ni salama na tulivu.Wanafunzi mbalimbali waliozungumza na Future Media Update wamepongeza jinsi zoezi hilo linavyofanyika kwa utulivu na ufanisi mkubwa, wakilinganisha na chaguzi zilizopita ambazo zilikuwa na changamoto mbalimbali. Mmoja wa wanafunzi alisema, "Mwaka huu tumeona mageuzi makubwa, kila kitu kinaenda kwa mpangilio mzuri na kwa uwazi."Akizungumza kwa msisitizo, Bi Salome Sengo – ambaye ni mhitimu wa JUCo na kwa sasa mwajiriwa chuoni hapo – ametoa rai kwa wanafunzi wote kuchukua jukumu lao la kidemokrasia kwa uzito mkubwa. Alisisitiza kuwa kura zao ndizo zitakazowapa viongozi bora watakaowatetea na kusimamia maslahi yao ndani ya chuo."Tunaamini katika sauti ya mwanafunzi. Na sauti hiyo ni kura yako. Jitokeze ukachague kiongozi anayeona mbali, anayejua matatizo yako na anayetaka kuyatatu," alisema Salome.Future Media Update itaendelea kukuletea taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu hadi mwisho wa mchakato.📡 #FutureMediaUpdate| Sauti ya Wanafunzi, Kazi Bila Mipaka
Comments