JUCo YATANGAZA UAMUZI MPYA KUHUSU INSTALLMENT YA NNE


 Juni 10, 2025 — Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan (JUCo) imetoa tamko rasmi kuhusu ulipaji wa faini (penalty) kwa wanafunzi walionufaika na mkopo wa elimu ya juu, hususan kwa malipo ya installment ya nne ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kufuatia kikao kilichofanyika tarehe 9 Juni 2025, kilichojumuisha viongozi wa juu wa chuo, pamoja na wawakilishi wa serikali ya wanafunzi na idara ya mikopo, uamuzi muhimu umetolewa kuhusu wanafunzi waliolipa ada zao kwa wakati.


Maamuzi hayo ni kama ifuatavyo:

• Wanafunzi waliokamilisha ada kati ya tarehe 1 Juni hadi 10 Juni 2025 wataondolewa penalty ya shilingi 25,000.

• Zoezi hili halitawahusu wanafunzi ambao hawajakamilisha malipo ya ada hadi sasa.

Katika hatua ya utekelezaji, wanufaika wote wa mkopo wametakiwa kufika katika Ofisi ya Afisa Mikopo kuanzia leo tarehe 10 Juni 2025 kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao, kama ilivyobainishwa kwenye taarifa hiyo.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Alimia Libela, kupitia kauli yake: “Kujenga Fursa Pamoja”, ameendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kusimamia maslahi ya wanafunzi na kuhakikisha haki zao zinalindwa kwa usawa.

Licha ya kuwa Amemaliza muda wake katika Uongozi.

Imeandikwa na Jeremia emanuel 


Comments