GARI LA MUZIKI LA CHADEMA LAPATA AJALI


 Gari la muziki iliyokuwa kwenye msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche imepata ajali alfajiri ya leo Juni 5, 2025 katika eneo la Msamvu Morogoro baada ya kuacha njia na kugonga lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara. 

Ajali hiyo imesababisha majeraha madogo kwa watu wanne waliokuwa ndani ya gari hiyo ya muziki akiwemo Twaha Mwaipaya, ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Nanguji mkoani Morogoro.

Comments