Mh. Daniel Augustino Atangaza Mageuzi Makubwa Serikalini – Awapa Siku1 Mawaziri Wastaafu Kuwasilisha Ripoti Mpya



Katika kikao rasmi cha kufungua Bunge la Serikali ya Wanafunzi, Mheshimiwa Daniel Augustino ametangaza mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kiutendaji ndani ya serikali ya wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo.

Akizungumza mbele ya wabunge na viongozi wa serikali ya wanafunzi, Mh. Augustino ameeleza kuwa Wizara ya Elimu imegawanywa rasmi kuwa wizara mbili tofauti:

• Wizara ya Elimu ya Juu – Itakayoshughulikia masuala ya wanafunzi wa degree.

• Wizara ya Elimu itakayo Shughulikia wanafunzi wa diploma(Stashahada)

Aidha, ameanzisha Wizara mpya ya Miundombinu, ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mazingira, vifaa na maendeleo ya kimazingira ndani ya Chuo.

Katika hatua nyingine, Mh. Augustino Ameikataa ripoti ya serikali iliyopita, akisema haikidhi vigezo vya uhalisia wa utendaji. Ameagiza serikali mpya kuwasilisha ripoti kamili ndani ya masaa saba (7) mbaka sa kumi jioni.

Kwa kuimarisha utulivu wa Uongozi, Mh. Augustino amesisitiza kuwa hakuna waziri atakayevuliwa madaraka baada ya kuapishwa, na kwamba uteuzi uliokamilika ni wa mwisho. Aliwaasa mawaziri na wabunge waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya wanafunzi wote.
   Imeandikwa na;
Jey Future Tz.
  (Future Media Update)


Comments