NITA KIMBIZANA NAO MWENYEWE



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Tundu Lissu ameileza mahakama kuwa yeye hajahukumiwa hukumu ya kifo lakini pamoja na kuwekwa eneo hilo kinyume cha sheria lakini bado pia haki zake za msiungi zinapuuzwa ikiwemo ya kuabudu pamoja na kufanya mazoezi.

“Ninakaa wapi? Gerezani, Gereza la Ukonga kuna sehemu moja inaitwa ‘special room’ eneo maalum ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, mimi ninakaa hiyo sehemu wanayokaa wanaosubiri kunyongwa (death rock).”— amesema Lissu.

“Sasa Mheshimwa ukiwa death rock maana yake ni nini? Kanuni ya 33 inazungumzia watu walio death rock inasema hivi: ukikaa death rock Mheshimwa kama ninachokaa mimi wakati sijahukumiwa kifo angalau bado sheria inasema wale waliohukumiwa kifo wanatakiwa watenganishwe na wafungwa wengine”

“Mimi nimekaa death rock tangu ljumaa Kuu mpaka leo, na nikitoka kuonana na mawakili wangu au ndugu zangu ninaambatana na askari wawili muda wote kama inavyotakiwa kwa waliohukumiwa kifo.”

“Ninalindwa muda wote, usiku na mchana, mimi sijahukumiwa kifo lakini ninakaa death rock pamoja na kuwa death rock bado una haki kwa mfano, haki ya kuabudu”— amesema Lissu.

Hata hivyo upande wa Jamhuri umeeleza kuwa haujapewa nafasi ya kusikilizwa kutokana na madai hayo lakini Hakimu Kiswaga amesema kuwa madai hayo yamebainishwa na mshtakiwa kama taarifa hivyo itafanyiwa kazi kiutawala.




Comments