PERNATY ZA ZUA TAHARUKI JUCO,WANAFUNZI WAPAZA SAUTI

 


Morogoro, Jordan University College – Malalamiko mazito yametanda miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Jordan University College (JUCo), baada ya idadi kubwa yao kupigwa penalty ya ada licha ya baadhi yao kuthibitisha kuwa walikamilisha malipo yao kwa wakati.

Taarifa za ndani kutoka kwa wanafunzi zinaeleza kuwa mfumo wa ada wa chuo hicho umeendelea kuonesha madeni kwa wanafunzi, huku wengine wakishtuka kuona kiasi cha shilingi elfu 25 kikiwasilishwa kama deni jipya hata baada ya kulipa ada kikamilifu.

"Nilimaliza kulipa ada jana, nikapewa taarifa kuwa deni langu ni sifuri. Lakini leo asubuhi napata taarifa kuwa nina deni la elfu 25. Hii inaumiza sana,” alisema mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa hofu ya madhara.

Mbali na waliokamilisha ada, malalamiko zaidi yanatoka kwa wanafunzi wanaotegemea mikopo ya serikali (boom) ili kulipia ada zao. Wengi wao wameshindwa kulipa kutokana na kuchelewa kwa fedha hizo, na sasa wanakabiliwa na hatari ya kuongezewa madeni kupitia penalty.

“Hatuwezi kulipa kabla ya kupata boom. Sasa kosa liko wapi hadi mtu apigwe penalty ya kuchelewa?” alihoji mwanafunzi mwingine anae chukua shahada ya sheria.

Wanafunzi hao wanasema kuwa hawajapewa ufafanuzi rasmi kutoka kwa uongozi wa chuo kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi na vigezo vinavyotumika kuamua penalty. Wameomba chuo kitoe taarifa ya haraka kwa kuwa hali hiyo inaongeza msongo wa mawazo hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho na wale wanaotegemea msaada wa kifedha kutoka kwa familia zao.

Mpaka sasa, juhudi za kuwasiliana na upande wa uongozi wa chuo kuhusu suala hili hazijazaa matunda,@FutureMediaupdate Bado tunaendelea kutafuta mawasiliano  ya uongozi chuoni hapo.


Comments