Polisi wa Minnesota na FBI wamsaka mshukiwa wa mauaji ya wabunge wa chama cha Democratic


   Polisi wa Minnesota na FBI wamsaka mshukiwa wa mauaji ya wabunge wa chama cha Democratic

Polisi wa jimbo la Minnesota kwa kushirikiana na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wameanzisha msako mkali dhidi ya mshukiwa anayehusishwa na mashambulizi ya risasi yaliyosababisha vifo vya wabunge wawili wa chama cha Democratic.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa, mshukiwa huyo anajulikana kama Vance Boelter, ambaye inadaiwa alijihami kwa bunduki na kisha kuwashambulia kwa makusudi wabunge hao waliokuwa nyumbani kwao.


Wabunge walioathirika ni:

       Melissa Hortman (miaka 55) – alifariki dunia akiwa nyumbani.Mark Hortman (miaka 58) – mume wake, alifariki dunia katika Hospitali ya North Memorial baada ya kufikishwa kwa ajili ya matibabu.

FBI imetangaza zawadi ya dola 50,000 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa mshukiwa huyo.

Tukio hili limeitikisa siasa za Minnesota na taifa kwa ujumla, likiwa ni sehemu ya msururu wa matukio ya vurugu yanayolenga wanasiasa katika siku za hivi karibuni.

Maafisa wa usalama wametoa wito kwa umma kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa yoyote muhimu na pia kuacha kuhudhuria maandamano yaliyopangwa na kundi la “No Kings”, kwa sababu za kiusalama.

Kwa sasa, hospitali ya Mercy imefungwa (lockdown) wakati uchunguzi unaendelea, huku polisi wakikusanya ushahidi zaidi.

Hali bado ni ya tahadhari katika maeneo mbalimbali ya Minnesota.


Comments