Rais na Makamu wa JUCSO Kuapishwa Ijumaa Hii

 


Kamati ya Uchaguzi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan (JUCO), kupitia taarifa rasmi iliyotolewa tarehe 11 Juni 2025, imewatangazia wanafunzi wote kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Serikali ya Wanafunzi JUCSO pamoja na Makamu wa Rais kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Kwa mujibu wa barua hiyo, hafla hiyo itafanyika Ijumaa tarehe 13 Juni 2025, katika Eneo la Block B, kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi.

Taarifa hiyo imetolewa na Bw. Ezekiel James Kayeni, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Huru ya Uchaguzi JUCO.

Comments