Tazama MCHEZAJI WA KLABU YA PSG, ALIYELALA KITANDANI HAJITAMBUI 'Coma' KWA MIAKA 39.

 ANAITWA 'Jean-Pierre Adams' 


Alifanyiwa upasuaji (surgery) wa mguu,lakini upasuaji huo ulienda ndivyo sivyo (ulikosewa) baada ya daktari mwenye dhamana kumzidishia dawa za usingizi na hivyo kumsababishia COMA (hali ya kutokujitambua na kushindwa kufanya jambo lolote)  Daktari aliye

Kosea alipigwa fain YA Tsh. million 1.7 tuu

Baada ya Makosa ya Daktari Katika Upasuaji Wake wa mguu  Mwaka 1982, Mchezaji wa Klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, Jean-Pierre Adams aliingia Kwenye Coma Iliyomfanya Asiamke Kuanzia Mwaka  1982 Mpaka  Leo umauti ulipomkuta.

Daktari Mhusika Alisimamishwa Kazi Mwezi Mmoja  na Faini ya Tsh. Mil 1.7 .

March 10, 1948 alizaliwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu za soka za Nice (1973-1977) na PSG (1977-1979) za Ufaransa Jean-Pierre Adams akicheza nafasi ya beki wa kati.

Jean alizaliwa huko Dakar Senegal kipindi ambacho nchi hiyo iko chini ya utawala wa Ufaransa, ni mwafrika. Alipotimiza umri wa miaka 10 yeye na bibi yake walihamia huko Montargis Ufaransa na kuendelea na maisha.

March 17, 1982 akiwa na miaka 34, Jean alifanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha ya kuumia mguu kwa akiwa uwanjani hali iliyopelekea alazwe katika hospitali ya Édouard Herriot huko Lyon, wakati huo alikuwa ameshastaafu soka.

Makosa yaliyofanywa na mtaalamu wa hospitali hiyo katika upasuaji wake yalipelekea Jean aingie kwenye Coma, na kuanzia mwaka huo wa 1982 mpaka hivi leo alipofariki dunia.

Katikati ya miaka ya 1990 mahakama ya sheria nchini humo ilitoa uamuzi juu ya kesi hiyo, Daktari aliyefanya kosa hilo la kitaalamu alipewa adhabu ya kusimamishwa kazi kwa mwezi mmoja na faini ya Dola $815 sawa na zaidi ya Tsh. Milioni 1.7 .

Jean leo hii amekutwa na umauti akiwa na umri wa miaka 73.Umauti ulimkuta akiwa bado yupo katika Coma kwa miaka 39 tangu alipofanyiwa upasuaji

Msaada pekee wa Jean kwa miaka yote 39 ni mke wake kipenzi Bernadette Adams aliyemuoa mwaka 1969 na kupata naye watoto wawili, Laurent (1969) na Frédéric (1976).



Bernadette mpaka mume wake anafariki alikua anaendelea kumfanyia mumewe sherehe mbalimbali kama siku za kuzaliwa. Jean-Pierre alikua hawezi kuwasiliana wala kuelezea chochote, lakini bado alikua anaweza kupumua, kuhisi, na kukohoa bila msaada wa vifaa vya matibabu na alikua anaishi nyumbani kwake Mjini Nimes.

Comments