TAZAMA NAMNA MFUMO WA KUZUIA MAKOMBORA UNAVYOTUMIA WA ISRAEL
Pichani juu ni mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel ikizuia makumi ya makombora ya masafa marefu kutoka Iran na chini ni matokeo ya madhara ya makombora machache yaliyofanikiwa kupenya na kutua
Iran inafanyaje kuupenya mfumo wa Iron Dome? Mfumo huo una kiwango maalumu cha idadi ya makombora unaoweza kuyazuia kwa wakati mmoja hivyo Iran inachofanya ni kurusha idadi kubwa zaidi ya makombora hayo ili yanayozidi yapenye hata hivyo Iron Dome inatajwa kwamba imeendelea kufanyiwa maboresho kuongeza idadi ya udhibiti wa pamoja.
Kiufupi Israel isingekuwa na mfumo huu thabiti wa ulinzi wa anga majengo yote yanayoonekana pichani yangekuwa majivu kutokana na wingi wa makombora yanayorushwa na Iran kwa wakati mmoja
Israel kwa sasa inalenga kukomesha uwezo wa Iran kuzalisha makombora hayo ya masafa marefu ambapo tayari usiku wa kuamkia jana katika mashambulizi yake ililenga pia kituo kikuu cha Iran cha programu ya uzalishaji wa makombora hayo ya kimkakati.
Comments