ZOEZI LA KUPIGA KURA JUCO LAFUNGWA RASMI, KURA ZAHESABIWA KWA UMAKINI MKUBWA
Jordan University College (JUCo) imemaliza rasmi zoezi la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi. Zoezi hilo limehitimishwa leo Jioni kwa mafanikio makubwa huku likishuhudiwa na ushiriki mkubwa wa wanafunzi waliokuwa na hamasa ya kuchagua viongozi watakaowawakilisha katika mwaka ujao wa masomo.
Kwa sasa, hatua ya kuhesabu kura inaendelea chini ya usimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Chuo, ambayo imesisitiza uadilifu, uwazi na haki katika kila hatua ya mchakato huo. Mwenyekiti wa tume ametoa wito kwa wanafunzi kuwa watulivu wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea, akiahidi kuwa matokeo yatatangazwa mara tu baada ya uhakiki kamili.
Wanafunzi mbalimbali waliowasiliana na Future Media Update
"wamesifu jinsi mchakato mzima wa upigaji kura ulivyotekelezwa kwa weledi na utulivu, wakieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umeweka viwango vipya vya utawala bora chuoni".
Future Media Update itaendelea kukufikishia taarifa za kina kuhusu maendeleo ya mchakato huu hadi kutangazwa kwa matokeo rasmi.
📡 #FutureMediaUpdate | Tunakupatia Kilicho Bora
✍🏽 Imeandikwa na: Jey Future TZ
Comments