AFARIKI DUNIA WAKATI AKICHEZA MCHEZO WA KUCHAPANA NA KAKA YAKE


 #MICHEZO:

 Jackson Kayoka (14) mkazi wa kijiji cha Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amefariki dunia baada ya kuchapwa fimbo na kaka yake Samweli Kayoka (16), wakati wakicheza michezo ya kuchapana fimbo.

Inasemekana kuwa wakati watoto hao walipokuwa wakicheza kwa kuchapana na fimbo, Marehemu alipigwa na fimbo sehemu za kichwani na kudondoka chini kisha kupoteza fahamu.

Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Romwald Kapele, amedai kuwa watoto hao ni wa familia moja, na kwamba katika mila za kabila la Wasukuma ni kawaida kwa watoto wa umri huo kucheza michezo ya namna hiyo.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Shadrack Masija, inaeleza kuwa Mtoto Samweli Kayoka, ambae ni kaka marehemu anashikiliwa kwa kuhusika na mauaji, Marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Mtenga muda mfupi baada ya tukio kujitokeza.

Comments