RASMI NDOA YA NOUMA NA SIMBA IMEFUNJIKA
INAELEZWA KUWA Mlinzi kutoka Burkina Faso, Valentin Nouma, ameagana rasmi na klabu ya Simba SC ya Tanzania baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja pekee.Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo ameondoka kwa uamuzi wake binafsi kufuatia kukosa nafasi ya mara kwa mara ya kucheza, jambo ambalo limeathiri nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso.
Kuondoka kwa Nouma kunakuja katika kipindi ambacho Simba SC inaendelea na mchakato wa kufanya maboresho ya kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Comments