SEMINA YA UJUZI KWA VIJANA 15/7


 Youth Power Organization kwa kushirikiana na wataalamu wa maendeleo ya vijana kutoka ndani na nje ya nchi, inayo furaha kuwakaribisha vijana wote nchini kushiriki katika Semina Maalum ya Mtandaoni (Webinar) itakayofanyika tarehe 15 Julai 2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ujuzi kwa Vijana Duniani (World Youth Skills Day) kama inavyotambuliwa na UNESCO.

      MADA KUU 

"Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali na Akili Bandia (AI) katika Kumuwezesha Kijana Kutengeneza Kipato"

Semina hii inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata maarifa ya kisasa juu ya namna ya kutumia teknolojia za kidijitali na akili bandia kama njia ya kujiajiri, kuunda miradi bunifu na kuongeza kipato katika mazingira ya sasa ya mabadiliko ya kidunia.

🧠 Watakaoshiriki

• Mtaalamu wa Kidijitali (Digital Expert)

• Afisa Maendeleo ya Jamii – Mkoa wa Morogoro

• Afisa Miradi – Save the Children (Tanzania Office)

• Mratibu wa Miradi – Restless Development Tanzania

            MUHIMU:

• Washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki bure vilivyosainiwa rasmi na Mkurugenzi wa Youth Power Organization.

• Vyeti hivi vinaweza kuwa sehemu muhimu ya CV yako, au vielelezo vya ushiriki katika shughuli za maendeleo ya vijana.

Semina hiyo itafanyika tarehe 15/7/ 2025,Muda ni saa 4:Ahsubuh mbaka sa 5 kamili Ahsubuh.

  TUKIO HILI LITAFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO(online)

Kupitia link itakayo tumwa kwe Channel hiyo hapo chini

www.youthpowerorganization.com/webinar



Comments