MUME AMNUNIA MKE WAKE KWA MIAKA 20,BAADA YA MKE WAKE KUMUUDHI
Mwanaume mmoja huko Japan, Otou Yumi hatimaye ameanza kuongea na mke wake baada ya kuamua kumnunia mke huyo kwa miaka 20. Kila aliposemeshwa na mke wake alikuwa haongei bali huitika kwa kichwa au kuguna.
Pamoja na kumnunia mke wake lakini Otou aliendelea kuhudumia familia yake na kuongea na watoto wake.
Mwanaume huyo alifikia uamuzi huo kwa madai kwamba mke wake alikuwa hamjali yupo bize na watoto.
Mtoto mkubwa wa mzee huyo aliamua kuchukua jukumu la kuwapatanisha kupitia kipindi cha televisheni na sasa wameanza kuongea.
Comments