Simba Day 2025: Ubunifu, Burudani na Soka kwa Kiwango cha Juu
Na Jeremia Emanuel – Uwanjani Benjamini Mkapa
Simba Day 2025 imeandika historia mpya jijini Dar es Salaam baada ya kushuhudia ubunifu wa hali ya juu, burudani ya kuvutia na mechi ya kirafiki iliyokusanya maelfu ya mashabiki.
Tukio hili, ambalo limekuwa utamaduni wa kila mwaka kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi, limeonesha kwa mara nyingine jinsi Simba SC inavyojua kuunganisha soka na burudani ya kisasa.Ahmed Ally Aingia kama “Traore”
Moja ya matukio yaliyotikisa uwanja huuni Namna msemaji wa Simba, Ahmed Ally,alivyo ingia uwanjani, ambaye alijitokeza kwa ubunifu wa hali ya juu akivalia mithili ya Traore. mwonekano uliopangwa kitaalamu uliamsha hisia kali kwa mashabiki. Mashabiki walishuhudia msemaji wao akibadilika na kuwa sehemu ya burudani, hali iliyoonesha uhalisia wa Simba Day kama jukwaa la ubunifu.Kabla ya Tukio hilo,Burudani ilipamba moto zaidi pale msanii maarufu Mbosso alipowasili uwanjani kwa sura isiyo ya kawaida, akionekana kama mhusika kutoka katika filamu ya Mad Max. Uvaaji wake, athari za mwonekano na namna alivyotoka na ujasiri uliwafanya mashabiki kujihisi kana kwamba wamehamishwa kwenye sinema halisi. Ni muunganiko wa muziki na uigizaji uliopelekea uwanja mzima kulipuka kwa shangwe.
Mashabiki na Mechi ya Kirafiki
Baada ya shamrashamra na burudani, uwanja uligeuka kuwa jukwaa la soka safi ambapo Simba SC ilikabiliana na Gor Mahia. Hii ilikuwa sehemu ya kumalizia kwa vitendo maadhimisho hayo, huku mashabiki wakipata ladha ya michezo sambamba na burudani.
Simba Day ya mwaka huu imeonesha wazi kuwa hafla hii imepiga hatua kubwa kimaudhui na kiubunifu. Kutoka kwa Ahmed Ally kuingia kama Traore hadi Mbosso kuigiza mithiri ya Mad Max, na kisha mechi ya kirafiki, yote yameacha kumbukumbu isiyosahaulika.
imeandikwa na Jeremia emanuel(FUTURE MEDIA UPDATE)
Comments